Durusu na Mazingatio kutokana na Suratul Hujuraati دروس وعبر من سورة الحجرات 🔴 LIVE | Ust Kassa
Darsa ilifanyika Shawwal 22, 1446 H Jumapili April 20, 2025
دروس وعبر من سورة الحجرات
Durusu na Mazingatio kutokana na Suratul Hujuraati
Umuhimu wa Suratul-Hujuraat
Suratil Hujuraat ni muhimu sana kwa sababu ya kanuni na maadili ya jumla ya Kiislamu, miongozo, na adabu za kimaadili iliyomo katika kiwango cha nafsi na jamii. Sura imemeweka mipaka ya mahusiano, imehifadhi haki za kila mwanadamu, na kuunda katiba kamili katika elimu, maadili na sheria.
Kupitia kwayo, inajenga jamii iliyo bora, yenye uaminifu inayofurahia tabia njema na ladha nzuri, pamoja na kufurahia hekima na busara na kutobebwa na uvumi na maneno bila ya kuthibitisha na kubainisha ukweli. Huu ndio wasiwasi wa umma wa Kiislamu unaohifadhi haki za Allah na haki za waja Wake.
Suratul-Hujuraat ina durusu -mafunzo- na mazingatioa -maadili- mengi:
1. Wajibu wa kutanguliza Amri ya Allah na ya Rasuli Wake; kwa kushikamana na Kitabu cha Allah na Sunnah za Rasuli Wake, na kwamba yana maamuzi na yenye kutawala katika maisha ya Muislamu, na yanatanguliza juu ya mila, desturi, na kadhalika.
2. Kuwafunza Waislamu baadhi ya maadili na adabu wanazopaswa kuwa nazo mbele ya Rasuli wa Allah katika jinsi ya kuamiliana naye, kuzungumza naye, na hata kumwita, ili kuitukuza hadhi yake ya utukufu na kuheshimu nafasi yake, kwani yeye si kama watu wa kawaida.
3. Kuadhimisha ibada ya kuleta suluhu -maupatanisho- baina ya Waislamu, kwa kutafuta njia munasaba za kuwapatanisha wale wanaohitilafiana, kwa kuzingatia dhana ya udugu unaowaunganisha.
4. Sura inabainisha maadili yanayotakiwa kujipamba nayo jamii ya Kiislamu, ambamo usalama na utu wa watu hauvunjwa kwa njia yoyote ile.
5. Surah inaonya dhidi ya dhihaka, masengenyo, kashfa, na kupachikana majina.
6. Surah inakataza kusengenya, kufanyiana ujasusi na kuwadhaniana.
7. Surah inaweka wazi kwamba Allah Aliumba viumbe kutokana na mwanamume na mwanamke, na akawagawanya katika mataifa na makabila kwa madhumuni ya kuishi pamoja na kuelewana, na si kwa ajili ya kubaguana na kujifakhari, iwe kwa nasaba au nchi.
8. Surah inabainisha kwamba kiwango cha ubora mbele ya Muumba ni uchamungu na si kitu kingine chochote kile.